Proverbs 12

Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii


1 aYeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa,
bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.


2 bMtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana,
bali Bwana humhukumu mwenye hila.


3 cMtu hathibitiki kutokana na uovu,
bali mwenye haki hataondolewa.


4 dMke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe,
bali aaibishaye ni kama uozo
katika mifupa ya mumewe.


5 Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki,
bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.


6 eManeno ya waovu huotea kumwaga damu,
bali maneno ya waadilifu huwaokoa.


7 fWatu waovu huondolewa na kutoweka,
bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.


8 gMtu husifiwa kulingana na hekima yake,
bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.


9 Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,
kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.


10 hMtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,
bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.


11 iYeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.


12 jWaovu hutamani mateka ya watu wabaya,
bali shina la mwenye haki hustawi.


13 kMtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,
bali mwenye haki huepuka taabu.


14 lKutokana na tunda la midomo yake
mtu hujazwa na mambo mema,
hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.


15 mNjia ya mpumbavu huonekana sawa
machoni pake mwenyewe,
bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.


16 nMpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja,
bali mtu wa busara hupuuza matukano.


17 oShahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,
bali shahidi wa uongo husema uongo.


18 pManeno ya kipumbavu huchoma kama upanga,
bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.


19 qMidomo isemayo kweli hudumu milele,
bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.


20 rUpo udanganyifu katika mioyo
ya wale ambao hupanga mabaya,
bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.


21 sHakuna dhara linalompata mwenye haki,
bali waovu wana taabu nyingi.


22 t Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,
bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.


23 uMtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe,
bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.


24 vMikono yenye bidii itatawala,
bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.


25 wMoyo wa wasiwasi humlemea mtu,
bali neno la huruma humfurahisha.


26 xMtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki,
bali njia ya waovu huwapotosha.


27 Mtu mvivu haoki mawindo yake,
bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.


28 yKatika njia ya haki kuna uzima;
katika mapito hayo kuna maisha ya milele.
Copyright information for SwhKC